Colossians 3

1Ikiwa tena Mungu amewafufua pamoja na Kristo, yatafuteni mambo ya juu ambako Kristo anakaa mkono wa kuume wa Mungu. 2Fikirini kuhusu mambo ya juu, sio kuhusu mambo ya duniani. 3Kwa kuwa mmekufa, na maisha yenu yamefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4Wakati Kristo atakapoonekana, ambaye ni maisha yenu, ndipo nanyi pia mtaonekana naye katika utukufu.

5Kwa hiyo yafisheni mambo yaliyo katika nchi yaani, zinaa, uchafu, shauku mbaya, nia mbaya, na tamaa, ambayo ni ibada ya sanamu. 6Ni kwa ajili ya mambo haya ghadhabu ya Mungu inakuja juu ya wana wasio tii. 7Ni kwa ajili ya mambo haya ninyi pia mlitembea kwayo mlipoishi kati yao. 8Lakini sasa ni lazima myaondoe mambo haya yote. Yaani, ghadhabu, hasira, nia mbaya, matusi, na maneno machafu yatokayo vinywani mwenu.

9Msidanganyane ninyi kwa ninyi, kwa kuwa mmeuvua utu wenu wa kale na matendo yake. 10Mmevaa utu mpya, ambao unafanywa upya katika maarifa kutokana mfano wa yule aliye muumba. 11Katika maarifa haya, hakuna Myunani na Myahudi, kutahiriwa na kutokutahiriwa, msomi, asiye msomi, mtumwa, asiye mtumwa, lakini badala yake Kristo ni mambo yote katika yote.

12Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13Chukulianeni ninyi kwa ninyi. Hurumianeni kila mtu na mwenzake. Kama mtu analalamiko dhidi ya mwingine, amsamehe kwa jinsi ilele ambayo Bwana alivyo wasamehe ninyi. 14Zaidi ya mambo haya yote, muwe na upendo, ambao ndio kigezo cha ukamilifu.

15Amani ya Kristo na iwaongoze mioyoni mwenu. Ilikuwa ni kwa ajili ya amani hii kwamba mliitiwa katika mwili mmoja. Iweni na shukrani. 16Na Neno la Kristo likae ndani yenu kwa utajiri. Kwa hekima yote, fundishaneni na kushauriana ninyi kwa ninyi kwa Zaburi, nyimbo, na nyimbo za rohoni. Imbeni kwa shukrani mioyo yenu kwa Mungu. 17Na chochote mfanyacho, katika maneno au katika matendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu. Mpeni shukrani Mungu baba kupitia Yeye.

18Wake, wanyenyekeeni waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. 19Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali dhidi yao. 20Watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, maana ndivyo impendezavyo Bwana. 21Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa.

22Watumwa, watiini mabwana zenu katika mwili kwa mambo yote, sio kwa huduma ya macho kama watu wa kufurahisha tu, bali kwa moyo wa kweli. Mwogopeni Mungu. 23Chochote mfanyacho, fanyeni kutoka nafsini mwenu kama kwa Bwana na si kama kwa wanadamu. 24Mnajua ya kwamba mtapokea tuzo ya umilkaji kutoka kwa Bwana. Ni Kristo Bwana mnayemtumikia. Kwa sababu yeyote atendaye yasiyo haki atapokea hukumu kwa matendo yasiyo haki aliyoyafanya, na hakuna upendeleo.

25

Copyright information for SwaULB